Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 66:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mbingu ni kiti changu cha enzi,dunia ni kiti cha kuwekea miguu yangu.Mtanijengea nyumba ya namna gani basi,Mahali nitakapoweza kupumzika?

2. Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote,na hivi vyote ni mali yangu.Lakini ninachojali mimini mtu mnyenyekevu na mwenye majuto,mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.

3. “Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka:Wananitolea tambiko ya ng'ombena mara wanaua watu kutambikia.Wananitolea sadaka ya mwanakondoona pia wanamvunja mbwa shingo.Wananitolea tambiko ya nafakana pia kupeleka damu ya nguruwe.Wanachoma ubani mbele yanguna kwenda kuabudu miungu ya uongo.Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.

4. Basi, nitawaletea taabu;yatawapata yaleyale wanayoyahofia;maana nilipoita hakuna aliyeitika,niliponena hawakusikiliza.Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu,walichagua yale ambayo hayanipendezi.”

5. Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,enyi msikiao neno lake mkatetemeka:“Ndugu zenu ambao wanawachukia,na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu,wamesema kwa dharau‘Mungu na aoneshe utukufu wake,nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!

6. Sikilizeni, ghasia kutoka mjini,sauti kutoka hekaluni!Hiyo ni sauti ya Mwenyezi-Munguakiwaadhibu maadui zake!

7. “Mji wangu mtakatifu,ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu;kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto.

8. Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo?Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo?Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja?Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja?Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu,alijifungua watoto wake.

9. Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe,halafu niwazuie wasizaliwe?Au mimi mwenye kuwajalia watoto,nitafunga kizazi chao?Mimi Mungu wenu nimesema.”

10. Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda!Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!

11. Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha,nanyi mtashiba kwa riziki zake;mtakunywa shibe yenu na kufurahi,kutokana na wingi wa fahari yake.

12. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakuletea fanaka nyingi kama mto,utajiri wa mataifa kama mto uliofurika.Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga,mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.

13. Kama mama amtulizavyo mwanawe,kadhalika nami nitawatuliza;mtatulizwa mjini Yerusalemu.

14. Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi;mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi.Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu,lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”

15. Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto,na magari yake ya vita ni kimbunga.Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali,na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.

Kusoma sura kamili Isaya 66