Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 49:9-18 Biblia Habari Njema (BHN)

9. kuwaambia wafungwa, ‘Tokeni humo gerezani’,na wale walio gizani, ‘Njoni nje mwangani!’Kila mahali watakapokwenda watapata chakulahata kwenye vilima vitupu watapata malisho.

10. Hawataona tena njaa wala kuwa na kiu.Upepo wa hari wala jua havitawachoma,mimi niliyewahurumia nitawaongozana kuwapeleka kwenye chemchemi za maji.

11. Milima yote nitaifanya kuwa njia,na barabara zangu kuu nitazitengeneza.

12. Watu wangu watarudi kutoka mbali,wengine kutoka kaskazini na magharibi,wengine kutoka upande wa kusini.”

13. Imbeni kwa furaha, enyi mbingu!Shangilia ewe dunia.Pazeni sauti mwimbe enyi milima,maana Mwenyezi-Mungu amewafariji watu wake,naam, atawaonea huruma watu wake wanaoteseka.

14. Wewe Siyoni wasema:“Mwenyezi-Mungu ameniacha;hakika Bwana wangu amenisahau.”

15. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya,asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake?Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe,mimi kamwe sitakusahau.

16. Nimekuchora katika viganja vyangu;kuta zako naziona daima mbele yangu.

17. Watakaokujenga upya wanakuja haraka,wale waliokuharibu wanaondoka.

18. Inua macho uangalie pande zote;watu wako wote wanakusanyika na kukujia.Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu,watu wako watakuwa kwako kama mapambo,utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.

Kusoma sura kamili Isaya 49