Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 46:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba,kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo;kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo.Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia,wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.

8. “Kumbukeni jambo hili na kutafakari,liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu.

9. Kumbukeni mambo niliyotenda hapo kale!Mimi ndimi Mungu na hakuna mwingine;naam, mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi.

10. Nilitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo,tangu kale nilitangaza mambo yatakayotukia.Lengo langu litatimia;mimi nitatekeleza nia yangu yote.

11. Ninamwita tai wangu kutoka mashariki,naam, msiri wangu kutoka nchi ya mbali.Mimi nimenena na nitayafanya;mimi nimepanga nami nitatekeleza.

12. “Nisikilizeni, enyi wenye vichwa vigumu,nisikilizeni enyi mlio mbali na ukombozi.

13. Siku ya kuwakomboa naileta karibu,haiko mbali tena;siku ya kuwaokoeni haitachelewa.Nitauokoa mji wa Siyoni,kwa ajili ya Israeli, fahari yangu.

Kusoma sura kamili Isaya 46