Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 46:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Wewe Beli umeanguka;Nebo umeporomoka.Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu.Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama,hao wanyama wachovu wamelemewa.

2. Nyinyi mmeanguka na kuvunjika,hamwezi kuviokoa vinyago vyenu;nyinyi wenyewe pia mtapelekwa uhamishoni!

3. “Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo,nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli.Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa;niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.

4. Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu;hata katika uzee wenu mimi nitawabeba.Nilifanya hivyo kwanza,nitafanya hivyo tena.Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.

5. “Mtanifananisha na nani, tufanane?Je, mwaweza kunilinganisha na nani, tulingane?

6. Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao,hupima fedha kwenye mizani zao,wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamukisha huisujudu na kuiabudu!

Kusoma sura kamili Isaya 46