Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 43:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Maana mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,Mungu Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wenu.Nitaitoa nchi ya Misri iwe fidia yenu,nitaitoa Kushi na Seba ili mwachwe huru.

4. Kwa vile mna thamani mbele yangu,kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda,mimi nawaacha watu kusudi niwapate nyinyi,nayaachilia mataifa badala ya maisha yenu.

5. Msiogope maana mimi nipo pamoja nanyi.“Nitawarudisha wazawa wenu toka mashariki,nitawakusanyeni kutoka magharibi.

6. Nitaiambia kaskazini, ‘Waache waondoke’,na kusini, ‘Usiwazuie’!Warudisheni watu kutoka mbali,kutoka kila mahali duniani.

7. Kila mmoja hujulikana kwa jina langu,niliwaumba wote na kuwafanyakwa ajili ya utukufu wangu.”

8. Waleteni mbele watu hao,ambao wana macho lakini hawaoniwana masikio lakini hawasikii!

9. Mataifa yote na yakusanyike,watu wote na wakutane pamoja.Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia?Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa?Wawalete mashahidi waokuthibitisha kwamba walifanya hivyo.Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”

10. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu;niliwachagua muwe watumishi wangu,mpate kunijua na kuniamini,kwamba ndimi peke yangu Mungu.Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine,wala hatakuwapo mungu mwingine.

11. “Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu,hakuna mkombozi mwingine ila mimi.

12. Nilitangaza yale ambayo yangetukia,kisha nikaja na kuwakomboa.Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo,nanyi ni mashahidi wangu.

13. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima.Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu;hakuna awezaye kupinga ninayofanya.”

14. Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu,Mtakatifu wa Israeli, asema hivi:“Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni.Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake,na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo.

15. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu;Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.”

Kusoma sura kamili Isaya 43