Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 42:16-25 Biblia Habari Njema (BHN)

16. “Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu,nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui.Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga,na mahali pa kuparuza patakuwa laini.Huo ndio mpango wangu wa kufanya,nami nitautekeleza.

17. Wote wanaotegemea sanamu za miungu,wote wanaoziambia: Nyinyi ni miungu yetu;watakomeshwa na kuaibishwa.

18. “Sikilizeni enyi viziwi!Tazameni enyi vipofu, mpate kuona!

19. Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu?Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu,au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

20. Nyinyi mmeona mambo mengi,lakini hamwelewi kitu.Masikio yenu yako wazi,lakini hamsikii kitu!”

21. Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya uaminifu wake,alipenda kukuza mwongozo wake na kuutukuza.

22. Lakini hawa ni watu walioibiwa mali na kuporwa!Wote wamenaswa mashimoni,wamefungwa gerezani.Wamekuwa kama mawindo bila mtu wa kuwaokoa,wamekuwa nyara na hakuna asemaye, “Waokolewe!”

23. Je, mtatega sikio kusikia kitu hiki?Nani kati yenu atakayesikiliza vizuri yatakayotukia?

24. Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao?Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao?Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea!Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake,wala hawakuzitii amri zake.

25. Kwa hiyo aliwamwagia hasira yake kali,akawaacha wakumbane na vita vikali.Hasira yake iliwawakia kila upande,lakini wao hawakuelewa chochote;iliwachoma, lakini hawakutilia jambo hilo maanani.

Kusoma sura kamili Isaya 42