Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 42:12-21 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Wote wakaao nchi za mbali,na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu.

13. Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa;kama askari vitani ajikakamua kupigana.Anapaza sauti kubwa ya vita,na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake.

14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza,nimekaa kimya na kujizuia;lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua,anayetweta pamoja na kuhema.

15. Nitaharibu milima na vilima,na majani yote nitayakausha.Mito ya maji nitaigeuza kuwa nchi kavu,na mabwawa ya maji nitayakausha.

16. “Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu,nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui.Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga,na mahali pa kuparuza patakuwa laini.Huo ndio mpango wangu wa kufanya,nami nitautekeleza.

17. Wote wanaotegemea sanamu za miungu,wote wanaoziambia: Nyinyi ni miungu yetu;watakomeshwa na kuaibishwa.

18. “Sikilizeni enyi viziwi!Tazameni enyi vipofu, mpate kuona!

19. Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu?Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu,au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

20. Nyinyi mmeona mambo mengi,lakini hamwelewi kitu.Masikio yenu yako wazi,lakini hamsikii kitu!”

21. Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya uaminifu wake,alipenda kukuza mwongozo wake na kuutukuza.

Kusoma sura kamili Isaya 42