Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 6:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “ ‘Twendeni, tukamrudie Mwenyezi-Mungu!Yeye mwenyewe ameturarua,lakini yeye mwenyewe atatuponya.Yeye mwenyewe ametujeruhi,lakini yeye mwenyewe atatibu majeraha yetu.

2. Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena,naam, siku ya tatu atatufufuaili tuweze kuishi pamoja naye.

3. Basi tumtambue,tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu.Kuja kwake ni hakika kama alfajiri,yeye atatujia kama manyunyu,kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”

Kusoma sura kamili Hosea 6