Agano la Kale

Agano Jipya

Ezra 2:63-70 Biblia Habari Njema (BHN)

63. Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka awepo kuhani atakayeweza kutoa kauli ya Urimu na Thumimu.

64. Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360;

65. mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.

66. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,

67. ngamia 435, na punda 6,720.

68. Watu hao waliotoka uhamishoni, walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu mjini Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa koo hizo walitoa matoleo ya hiari ili kusaidia ujenzi wa nyumba ya Mungu katika Yerusalemu.

69. Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani.

70. Basi, makuhani, Walawi na baadhi ya watu wengine wakaanza kuishi mjini Yerusalemu na katika vitongoji vyake. Nao waimbaji, walinzi wa hekalu na watumishi wa hekalu wakaanza kuishi katika miji yao; Waisraeli wote waliishi katika miji yao.

Kusoma sura kamili Ezra 2