Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 8:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Basi, Mungu akaniambia, “Wewe mtu, je, waona mambo wanayofanya, machukizo makubwa wanayofanya Waisraeli ili wapate kunifukuza kutoka maskani yangu? Tena utaona machukizo mengine makubwa zaidi.”

7. Kisha akanipeleka mpaka lango la ua. Nilipoangalia nikaona tundu ukutani.

8. Naye akaniambia, “Wewe mtu, toboa ukuta huu.” Nami, nikatoboa, nikaona kulikuwa na mlango.

9. Naye akaniambia, “Ingia ndani ukaangalie machukizo mabaya wanayofanya humo.”

10. Basi, nikaingia, nikaona sanamu za wadudu na za wanyama wa kila aina ya kuchukiza na vinyago vyote vya miungu ya Waisraeli, vimechorwa kuuzunguka ukuta.

11. Na mbele ya sanamu hizo walisimama wazee sabini wa watu wa Israeli pamoja na Yaazania mwana wa Shafani. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi, na moshi wa ubani ulipanda juu.

Kusoma sura kamili Ezekieli 8