Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 33:27-30 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.

28. Nitaifanya nchi kuwa jangwa na tupu. Mashujaa wake wenye kiburi nitawaua. Milima ya Israeli itakuwa jangwa na hakuna mtu atakayepita huko.

29. Naam, nitakapoifanya hiyo nchi kuwa jangwa na tupu kwa sababu ya mambo yote ya kuchukiza waliyotenda, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

30. Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Wananchi wenzako wanazungumza juu yako, wameketi kutani na milangoni mwa nyumba zao na kuambiana: ‘Haya! Twende tukasikie neno alilosema Mwenyezi-Mungu!’

Kusoma sura kamili Ezekieli 33