Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 30:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Toa unabii useme kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Ombolezeni na kusema: ‘Ole wetu siku ile!’

3. Kwa maana, siku hiyo imekaribia;siku ile ya Mwenyezi-Mungu iko karibu.Hiyo itakuwa siku ya mawingu,siku ya maangamizi kwa mataifa.

4. Vita vitazuka dhidi ya Misri,na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi,wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa,mali zao zitakapochukuliwa,na misingi ya miji yao kubomolewa.

5. “Watu wote waliofungamana na Wamisri, yaani watu wa Kushi, Puti, Ludi, Arabia yote na Libia wataangamia pamoja nao.

6. “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Wote wanaoiunga mkono Misri wataangamia,mashujaa wake wenye fahari wataangamizwa,tangu Migdoli mpaka Syene watu watauawa vitani.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.

7. Misri itakuwa jangwa kama nchi zilizo jangwana miji yake itakuwa magofu kama miji iliyoteketezwa.

8. Nitakapoiteketeza Misri kwa motona kuwavunjilia mbali wasaidizi wake wotendipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

9. Siku hiyo, nitapeleka wajumbe kwenda kuwatishaWaethiopia wanaojidhani kuwa salama.Watatetemeka siku Misri itakapoangamia.Naam! Kweli siku hiyo yaja!

10. “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Nitamtumia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni,kukomesha utajiri wa nchi ya Misri.

11. Nebukadneza mwenyewe pamoja na watu wake,taifa katili kuliko mataifa yote,watatumwa kuiangamiza nchi ya Misri.Watachomoa panga zao dhidi ya Misrina kuijaza nchi hiyo watu waliouawa.

Kusoma sura kamili Ezekieli 30