Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 17:35-41 Biblia Habari Njema (BHN)

35. Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya agano nao na kuwaamuru, “Msiabudu miungu mingine; msiisujudie, msiitumikie wala msiitambikie.

36. Mtaniabudu mimi Mwenyezi-Mungu, ambaye niliwatoa huko Misri kwa uwezo na nguvu nyingi. Mtanisujudia mimi na kunitolea sadaka.

37. Wakati wote mtatii masharti, maongozi, sheria na amri ambazo niliandika kwa ajili yenu, siku zote mtakuwa waangalifu kuzitenda. Msiiabudu miungu mingine,

38. wala msisahau agano nililofanya nanyi; msiiabudu miungu mingine, bali

39. mtaniabudu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nami nitawaokoa kutoka mikononi mwa adui zenu.”

40. Lakini watu hao hawakusikiliza, bali waliendelea kutenda kama walivyofanya hapo awali.

41. Basi mataifa haya yalimwabudu Mwenyezi-Mungu, lakini pia yalitumikia sanamu zao za kusubu; na mpaka sasa hivi, wazawa wao wanaendelea kutenda hivyo kama walivyotenda babu zao.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 17