Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wafalme 14:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wakati huo, Abiya mwana wa mfalme Yeroboamu, akawa mgonjwa.

2. Yeroboamu akamwambia mkewe, “Jisingizie kuwa mwingine, uende mjini Shilo anakokaa nabii Ahiya aliyesema kwamba mimi nitakuwa mfalme wa Israeli.

3. Mpelekee mikate kumi, maandazi kadha, na asali chupa moja. Yeye atakuambia yatakayompata mtoto wetu.”

4. Basi, mkewe Yeroboamu akaondoka, akaenda Shilo nyumbani kwa Ahiya. Wakati huo, Ahiya alikuwa hawezi tena kuona sawasawa kwa sababu ya uzee.

Kusoma sura kamili 1 Wafalme 14