Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 7:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Uzi alikuwa na mwana mmoja, jina lake Izrahia. Na wana wa Izrahia walikuwa Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia, jumla wanne, na wote walikuwa wakuu wa jamaa.

4. Kwa vile ambavyo wake na watoto wao walikuwa wengi sana, mliweza kupatikana vikosi vya wanajeshi 36,000 kutokana na wazawa wao.

5. Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikishwa kwa kufuata koo, walikuwa 87,000, na wote walikuwa mashujaa wa vita.

6. Benyamini alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 7