Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 5:11-26 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Kabila la Gadi lilipakana na kabila la Reubeni upande wa kaskazini, katika nchi ya Bashani iliyoenea mashariki hadi Saleka.

12. Yoeli ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa ukoo ulioongoza, wa pili Shafamu. Yanai na Shefati walikuwa waanzilishi wa koo nyingine huko Bashani.

13. Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba: Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yaakani, Zia na Eberi.

14. Wote hawa walikuwa wana wa Abihaili, aliyekuwa mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi.

15. Ahi, aliyekuwa mwana wa Abdieli na mjukuu wa Guni, alikuwa mkuu katika koo hizi.

16. Waliishi katika sehemu ya Gileadi, katika Bashani na miji yake na katika malisho yote ya Sharoni, hadi mipakani.

17. Watu hao wote waliandikishwa katika koo, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na Yeroboamu, mfalme wa Israeli.

18. Makabila ya Reubeni, Gadi na Manase ya mashariki, yalikuwa na wanajeshi shupavu wapatao 44,760, wenye ngao na mapanga, wavuta pinde stadi vitani.

19. Walipigana vita na makabila ya Wahajiri, Yeturi, Nafishi na Nodabu.

20. Waliweka tumaini lao kwa Mungu na wakamwomba awasaidie, naye akaitikia ombi lao na kuwatia mikononi mwao Wahajiri pamoja na marafiki zao.

21. Waliteka nyara ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000 na mateka hai 100,000.

22. Waliua maadui wengi sana kwa sababu vita hivyo vilikuwa ni vita vya Mungu. Nao waliendelea kuishi katika nchi hiyo, mpaka wakati wa uhamisho.

23. Watu wa Manase ya mashariki waliishi katika nchi ya Bashani. Idadi yao iliongezeka kwa wingi sana, wakasambaa upande wa kaskazini hadi Baal-hermoni, Seniri na mlima Hermoni.

24. Wafuatao ndio waliokuwa wakuu wa koo za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yadieli. Wote walikuwa askari shujaa, watu mashuhuri sana na viongozi katika koo hizo.

25. Lakini watu walimwasi Mungu wa babu zao, wakafanya uzinzi kwa kuabudu miungu ya wakazi wa nchi hizo ambazo Mungu aliziangamiza mbele yao.

26. Basi, Mungu wa Israeli akamfanya Pulu, mfalme wa Ashuru, (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-pileseri), aivamie nchi yao na kuwachukua mateka hao Wareubeni, Wagadi na nusu Manase ya mashariki mpaka uhamishoni huko Hala, Habori na Hara, kando ya mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 5