Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 4:5-13 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Ashuru, mwanzilishi wa mji wa Tekoa, alikuwa na wake wawili: Hela na Naara.

6. Naara alimzalia wana wanne: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.

7. Hela alimzalia wana watatu: Serethi, Ishari na Ethnani.

8. Hakosi aliwazaa Anubi na Sobeba, na ndiye aliyekuwa baba wa jamaa za wazawa wa Aharheli, mwana wa Harumu.

9. Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yabesi, aliyeheshimiwa kuliko ndugu zake wote. Mama yake alimpa jina la Yabesi kwa sababu alimzaa kwa maumivu.

10. Lakini Yabesi alimwomba Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, nakusihi unibariki na kuipanua mipaka yangu. Mkono wako uwe pamoja nami na unilinde kutokana na jambo lolote ovu, lisiniumize.” Naye Mungu akamjalia yale aliyoomba.

11. Kelubu, nduguye Shuha, alimzaa Mehiri na Mehiri akamzaa Eshtoni.

12. Eshtoni alikuwa na wana watatu: Beth-rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa mwanzilishi wa mji wa Ir-nahashi. Wazawa wa watu hawa waliishi Reka.

13. Wana wa Kenazi walikuwa: Othnieli na Seraya; na wana wa Othnieli walikuwa Hathathi na Meonothai.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 4