Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 25:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi.

2. Wana wanne wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania na Asharela. Wao walikuwa chini ya uongozi wa Asafu aliyetabiri wakati wote chini ya uongozi wa mfalme.

3. Wana sita wa Yeduthuni: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia na Matithia. Wao walikuwa chini ya uongozi wa baba yao; na walitabiri kwa kutumia vinubi, na wakamshukuru na kumtukuza Mwenyezi-Mungu.

4. Wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.

5. Mungu alimpa Hemani, mwonaji wa mfalme, hawa watoto wa kiume kumi na wanne, na wa kike watatu, kama alivyoahidi ili kumtukuza.

6. Wanawe wote walipiga muziki kwa matoazi, vinanda na vinubi, kwenye ibada katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakiwa chini ya uongozi wa baba yao. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya amri ya mfalme.

7. Idadi yao pamoja na wale ndugu zao Walawi waliofundishwa kumwimbia Mwenyezi-Mungu, wote waliokuwa stadi, ilikuwa 288.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 25