Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 20:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika,

2. wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?”

3. Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali:

4. Mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”

5. Lakini wao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitoka kwa Mungu, yeye atatuuliza: ‘Mbona hamkumsadiki?’

6. Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii.”

7. Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.”

8. Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”

9. Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.

10. Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu.

11. Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.

12. Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.

13. Yule mwenye shamba akafikiri: ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.’

Kusoma sura kamili Luka 20