Agano la Kale

Agano Jipya

Neh. 3:7-13 Swahili Union Version (SUV)

7. Na baada yao wakafanyiza Melatia, Mgibeoni, na Yadoni, Mmeronothi, watu wa Gibeoni, na wa Mispa, raia wa kiti cha enzi cha liwali wa ng’ambo ya Mto.

8. Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.

9. Na baada yao akafanyiza Refaya, mwana wa Huri, akida wa nusu ya Yerusalemu.

10. Na baada yao akafanyiza Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akafanyiza Hatushi, mwana wa Hashabneya.

11. Malkiya, mwana wa Harimu, na Hashubu, mwana wa Pahath-moabu, wakafanyiza sehemu nyingine, na mnara wa tanuu.

12. Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.

13. Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa.

Kusoma sura kamili Neh. 3