Agano la Kale

Agano Jipya

Mhu. 4:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.

2. Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado;

3. naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.

4. Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.

5. Mpumbavu huikunja mikono yake,Naye hula chakula chake mwenyewe;

6. Heri konzi moja pamoja na utulivu,Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;na kujilisha upepo.

7. Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.

8. Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.

Kusoma sura kamili Mhu. 4