Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 4:2-21 Swahili Union Version (SUV)

2. (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,)

3. aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.

4. Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.

5. Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.

6. Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.

7. Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.

8. Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.

9. Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.)

10. Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.

11. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?

12. Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?

13. Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

14. walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

15. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.

16. Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa.

17. Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume;

18. kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.

19. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!

20. Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

Kusoma sura kamili Yn. 4