Agano la Kale

Agano Jipya

Ebr. 5:5-14 Swahili Union Version (SUV)

5. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,Ndiwe mwanangu,Mimi leo nimekuzaa.

6. kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani mileleKwa mfano wa Melkizedeki.

7. Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

8. na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;

9. naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

10. kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

11. Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

12. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

13. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

14. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

Kusoma sura kamili Ebr. 5