Agano la Kale

Agano Jipya

Ebr. 13:6-19 Swahili Union Version (SUV)

6. Hata twathubutu kusema,Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?

7. Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.

8. Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

9. Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.

10. Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.

11. Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.

12. Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango.

13. Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake.

14. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

15. Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

16. Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

17. Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

18. Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.

19. Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi.

Kusoma sura kamili Ebr. 13