Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 8:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,binadamu ni nini hata umjali?

5. Umemfanya awe karibu kama Mungu,umemvika fahari na heshima.

6. Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote;uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake:

7. Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini;

8. ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.

9. Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,kweli jina lako latukuka duniani kote!

Kusoma sura kamili Zaburi 8