Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 6:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako;usiniadhibu kwa ghadhabu yako.

2. Unihurumie, ee Mwenyezi-Mungu, nimeishiwa nguvu;uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nataabika mpaka mifupani.

3. Ninahangaika sana rohoni mwangu.Ee Mwenyezi-Mungu, utakawia mpaka lini?

4. Unigeukie, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe;unisalimishe kwa sababu ya fadhili zako.

5. Huko kwa wafu hakuna anayekukumbuka;huko kuzimu ni nani awezaye kukusifu?

6. Niko hoi kwa kilio cha uchungu;kila usiku nalowesha kitanda changu kwa machozi;kwa kulia kwangu naulowesha mto wangu.

7. Macho yangu yamechoka kwa huzuni;yamefifia kwa kutaabishwa na adui.

8. Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu!Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.

Kusoma sura kamili Zaburi 6