Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 5:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu,usikie ninavyopiga kite.

2. Usikilize kilio changu,Mfalme wangu na Mungu wangu,maana wewe ndiwe nikuombaye.

3. Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu,asubuhi nakutolea tambiko yangu,kisha nangojea unijibu.

4. Wewe si Mungu apendaye ubaya;kwako uovu hauwezi kuwako.

5. Wenye majivuno hawastahimili mbele yako;wewe wawachukia wote watendao maovu.

6. Wawaangamiza wote wasemao uongo;wawachukia wauaji na wadanganyifu.

7. Lakini, kwa wingi wa fadhili zako,mimi nitaingia nyumbani mwako;nitakuabudu kuelekea hekalu lako takatifu,nitakusujudia kwa uchaji.

8. Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako,maana maadui zangu ni wengi;uiweke njia yako wazi mbele yangu.

Kusoma sura kamili Zaburi 5