Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 42:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana;nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku,nimwombe Mungu anipaye uhai.

9. Namwambia Mungu, mwamba wangu:“Kwa nini umenisahau?Yanini niende huko na huko nikiombolezakwa kudhulumiwa na adui yangu?”

10. Nimepondwa kwa matukano yao,wanaponiuliza kila siku:“Yuko wapi, Mungu wako!”

11. Mbona nasononeka hivyo moyoni?Kwa nini nahangaika hivyo?Nitamtumainia Mungu,maana nitamsifu tena Mungu,aliye msaada wangu na Mungu wangu.

Kusoma sura kamili Zaburi 42