Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 42:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mbona nasononeka hivyo moyoni?Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu?Nitamtumainia Mungu,maana nitamsifu tenayeye aliye msaada wangu na Mungu wangu.

6. Nimesongwa na huzuni moyoni mwangu,kwa hiyo ninakukumbuka wewe, ee Mungu,kutoka katika eneo la Yordani,kutoka mlima Hermoni na Mizari.

7. Nimeporomoshewa mafuriko ya majimafuriko ya maji yaja karibunayo yaita maporomoko mapya.Mawimbi na mapigo yako yamenikumba.

8. Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana;nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku,nimwombe Mungu anipaye uhai.

9. Namwambia Mungu, mwamba wangu:“Kwa nini umenisahau?Yanini niende huko na huko nikiombolezakwa kudhulumiwa na adui yangu?”

10. Nimepondwa kwa matukano yao,wanaponiuliza kila siku:“Yuko wapi, Mungu wako!”

Kusoma sura kamili Zaburi 42