Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 40:8-15 Biblia Habari Njema (BHN)

8. kutimiza matakwa yako, ee Mungu wangu ni furaha yangu,sheria yako naishika kwa moyo wangu wote!”

9. Nimesimulia habari njema za ukombozi,mbele ya kusanyiko kubwa la watu.Kama ujuavyo ee Mwenyezi-Mungu,mimi sikujizuia kuitangaza.

10. Sikuuficha moyoni mwangu ukombozi ulionijalia,nimetangaza daima kuwa wewe ni mwokozi mwaminifu;sikulificha kusanyiko kubwa la watufadhili zako na uaminifu wako.

11. Ee Mwenyezi-Mungu, usininyime huruma yako!Fadhili zako na uaminifu wako vinihifadhi daima.

12. Maafa yasiyohesabika yanizunguka,maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona;ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu,nami nimevunjika moyo.

13. Upende ee Mwenyezi-Mungu kuniokoa;ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia.

14. Wanaonuia kuniangamiza,na waaibike na kufedheheka!Hao wanaotamani niumie,na warudi nyuma na kuaibika!

15. Hao wanaonisimanga,na wapumbazike kwa kushindwa kwao!

Kusoma sura kamili Zaburi 40