Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 40:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Ee Mwenyezi-Mungu, usininyime huruma yako!Fadhili zako na uaminifu wako vinihifadhi daima.

12. Maafa yasiyohesabika yanizunguka,maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona;ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu,nami nimevunjika moyo.

13. Upende ee Mwenyezi-Mungu kuniokoa;ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia.

14. Wanaonuia kuniangamiza,na waaibike na kufedheheka!Hao wanaotamani niumie,na warudi nyuma na kuaibika!

15. Hao wanaonisimanga,na wapumbazike kwa kushindwa kwao!

16. Lakini wote wale wanaokutafutawafurahi na kushangilia kwa sababu yako.Wapendao wokovu wako,waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!”

17. Mimi ni maskini na fukara, ee Bwana;lakini ee Bwana wewe wanikumbuka.Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;uje, ee Mungu wangu, usikawie!

Kusoma sura kamili Zaburi 40