Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 4:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo.Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia;unionee huruma na kusikia sala yangu.

2. Jamani, mtaniharibia jina langu mpaka lini?Mpaka lini mtapenda upuuzi na kusema uongo?

3. Jueni kuwa Mwenyezi-Mungu amejiteulia mwaminifu wake.Mwenyezi-Mungu husikia kila ninapomwomba.

4. Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi;tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.

5. Toeni tambiko zilizo sawa,na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.

6. Wengi husema: “Laiti tungepata tena fanaka!Utuangalie kwa wema, ee Mwenyezi-Mungu!”

7. Lakini mimi umenijalia furaha kubwa moyoni,kuliko ya hao walio na divai na ngano kwa wingi.

8. Nalala na kupata usingizi kwa amani;ee Mwenyezi-Mungu, wewe peke yako waniweka salama.

Kusoma sura kamili Zaburi 4