Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 38:14-22 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,kama mtu asiye na chochote cha kujitetea.

15. Lakini ninakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu;wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu.

16. Nakuomba tu maadui wasinisimange,wasione fahari juu ya kuanguka kwangu.

17. Karibu sana nitaanguka;nakabiliwa na maumivu ya daima.

18. Naungama uovu wangu;dhambi zangu zanisikitisha.

19. Maadui zangu hawajambo, wana nguvu;ni wengi mno hao wanaonichukia bure.

20. Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu,wananipinga kwa sababu natenda mema.

21. Usinitupe, ee Mwenyezi-Mungu;ee Mungu wangu, usikae mbali nami.

22. Uje haraka kunisaidia;ewe Mwenyezi-Mungu, uliye wokovu wangu.

Kusoma sura kamili Zaburi 38