Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 36:2-12 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Mwovu hujipendelea mwenyewe,hufikiri uovu wake hautagunduliwa na kulaaniwa.

3. Kila asemacho ni uovu na uongo;ameacha kutumia hekima na kutenda mema.

4. Alalapo huwaza kutenda maovu,hujiweka katika njia isiyo njema,wala haachani na uovu.

5. Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni;uaminifu wako wafika mawinguni.

6. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa,hukumu zako ni kama vilindi vya bahari.Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama

7. Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako!Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako.

8. Wawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako;wawanywesha kutoka mto wa wema wako.

9. Wewe ndiwe asili ya uhai;kwa mwanga wako twaona mwanga.

10. Uendelee kuwafadhili wale wanaokutambua;uzidi kuwa mwema kwa wanyofu wa moyo.

11. Usikubali wenye majivuno wanivamie,wala watu waovu wanikimbize.

12. Kumbe watendao maovu wameanguka;wameangushwa chini, hawawezi kuinuka.

Kusoma sura kamili Zaburi 36