Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 34:10-21 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa;lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.

11. Njoni enyi vijana mkanisikilize,nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu.

12. Je, watamani kufurahia maisha,kuishi maisha marefu na kufurahia mema?

13. Basi, acha kusema mabaya,na kuepa kusema uongo.

14. Jiepushe na uovu, utende mema;utafute amani na kuizingatia.

15. Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu,na kusikiliza malalamiko yao;

16. lakini huwapinga watu watendao maovu,awafutilie mbali kutoka duniani.

17. Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia,na kuwaokoa katika taabu zao zote.

18. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo;huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

19. Mateso ya mwadilifu ni mengi,lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote.

20. Huvilinda viungo vya mwili wake wote,hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.

21. Ubaya huwaletea waovu kifo;wanaowachukia waadilifu wataadhibiwa.

Kusoma sura kamili Zaburi 34