2. Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa zeze;mwimbieni kwa kinubi cha nyuzi kumi.
3. Mwimbieni wimbo mpya;pigeni kinubi vizuri na kushangilia.
4. Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli;na matendo yake yote ni ya kuaminika.
5. Mungu apenda uadilifu na haki,dunia imejaa fadhili za Mwenyezi-Mungu.
6. Mbingu ziliumbwa kwa neno la Mwenyezi-Mungu,na vyote vilivyomo kwa pumzi ya mdomo wake.
7. Alikusanya maji ya bahari kama katika chupa,vilindi vya bahari akavifunga ghalani.
8. Dunia yote na imwogope Mwenyezi-Mungu!Wakazi wote duniani, wamche!
9. Maana alisema na ulimwengu ukawako;alitoa amri nao ukajitokeza.
10. Mwenyezi-Mungu hupangua mipango ya mataifa,na kuyatangua mawazo yao.
11. Mpango wa Mwenyezi-Mungu hudumu milele;maazimio yake yadumu vizazi vyote.