16. Mfalme hawezi kuokolewa kwa kuwa na jeshi kubwa;wala shujaa hapati ushindi kwa nguvu zake kubwa.
17. Farasi wa vita hafai kitu kwa kupata ushindi;nguvu zake nyingi haziwezi kumwokoa mtu.
18. Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao,watu ambao wanatumainia fadhili zake.
19. Yeye huwaokoa katika kifo,huwaweka hai wakati wa njaa.
20. Mioyo yetu yamtumainia Mwenyezi-Mungu.Yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21. Naam twafurahi kwa sababu yake;tuna matumaini katika jina lake takatifu.
22. Fadhili zako zikae nasi, ee Mwenyezi-Mungu,kwani sisi tumekuwekea tumaini letu.