1. Ee Mwenyezi-Mungu, nakutukuza maana umeniokoa,wala hukuwaacha maadui zangu wanisimange.
2. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu,nilikulilia msaada, nawe ukaniponya.
3. Ee Mwenyezi-Mungu, umeniokoa kutoka kuzimu;umenipa tena uhai,umenitoa miongoni mwa waendao kuzimu.
4. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa, enyi waaminifu wake;kumbukeni utakatifu wake na kumshukuru.
5. Hasira yake hudumu kitambo kidogo,wema wake hudumu milele.Kilio chaweza kuwapo hata usiku,lakini asubuhi huja furaha.
6. Mimi nilipofanikiwa, nilisema:“Kamwe sitashindwa!”