Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 29:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima enyi viumbe vya mbinguni,semeni Mwenyezi-Mungu ni mtukufu na mwenye nguvu.

2. Semeni jina la Mwenyezi-Mungu ni tukufu.Mwabuduni katika mahali pake patakatifu.

3. Sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya maji;Mungu mtukufu angurumisha radi,sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya bahari!

4. Sauti ya Mwenyezi-Mungu ina nguvu,sauti ya Mwenyezi-Mungu imejaa fahari.

5. Sauti ya Mwenyezi-Mungu huvunja mierezi;Mwenyezi-Mungu avunja mierezi ya Lebanoni.

6. Huirusha milima ya Lebanoni kama ndama,milima ya Sirioni kama mwananyati.

7. Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutoa miali ya moto.

8. Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa,Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa la Kadeshi.

9. Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule,hukwanyua majani ya miti msituni,na hekaluni mwake wote wasema:“Utukufu kwa Mungu!”

10. Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika;Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.

11. Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu!Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!

Kusoma sura kamili Zaburi 29