7. Usikie, ee Mwenyezi-Mungu, ninapokulilia,unionee huruma na kunijibu.
8. Moyo wangu waniambia: “Njoo umtafute Mungu!”Basi, naja kwako, ee Mwenyezi-Mungu.
9. Usiache kuniangalia kwa wema.Usinikatae kwa hasira mimi mtumishi wako;wewe umekuwa daima msaada wangu.Usinitupe wala usiniache, ee Mungu Mwokozi wangu.
10. Hata kama wazazi wangu wakinitupa,Mwenyezi-Mungu atanipokea kwake.
11. Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu;uniongoze katika njia iliyo sawa,kwa sababu ya maadui zangu.
12. Usiniache maadui wanitende wapendavyo;maana mashahidi wa uongo wananikabili,nao wanatoa vitisho vya ukatili.
13. Naamini nitauona wema wake Mwenyezi-Mungukatika makao ya walio hai.
14. Mtegemee Mwenyezi-Mungu!Uwe na moyo, usikate tamaa!Naam, mtegemee Mwenyezi-Mungu!