Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 27:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu,ni nani nitakayemwogopa?Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu,sitamwogopa mtu yeyote.

2. Waovu wakinishambulia,na kutaka kuniangamiza,hao wapinzani wangu watajikwaa na kuanguka.

3. Hata jeshi likinizunguka,moyo wangu hautaogopa kitu;hata nikikabiliwa na vita,bado nitakuwa na tumaini.

4. Jambo moja nimemwomba Mwenyezi-Mungu,nalo ndilo ninalolitafuta:Nikae nyumbani mwa Mwenyezi-Mungusiku zote za maisha yangu;niuone uzuri wake Mwenyezi-Mungu,na kutafuta maongozi yake hekaluni mwake.

5. Siku ya taabu atanificha bandani mwake;atanificha katika hema lake,na kunisalimisha juu ya mwamba.

6. Nami kwa fahari nitaangalia juuya maadui zangu wanaonizunguka.Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake,nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.

7. Usikie, ee Mwenyezi-Mungu, ninapokulilia,unionee huruma na kunijibu.

8. Moyo wangu waniambia: “Njoo umtafute Mungu!”Basi, naja kwako, ee Mwenyezi-Mungu.

9. Usiache kuniangalia kwa wema.Usinikatae kwa hasira mimi mtumishi wako;wewe umekuwa daima msaada wangu.Usinitupe wala usiniache, ee Mungu Mwokozi wangu.

10. Hata kama wazazi wangu wakinitupa,Mwenyezi-Mungu atanipokea kwake.

Kusoma sura kamili Zaburi 27