Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 25:9-22 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu;naam, huwafundisha hao njia yake.

10. Mwenyezi-Mungu hutenda kwa fadhili na uaminifu,kwa wale wanaoshika agano lake na maamuzi yake.

11. Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu,unisamehe kosa langu kwani ni kubwa.

12. Kila mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu,Mwenyezi-Mungu atamfunza njia ya kufuata.

13. Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima,na wazawa wake watamiliki nchi.

14. Mwenyezi-Mungu ni rafiki ya wale wamchao;yeye huwajulisha hao agano lake.

15. Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima;yeye atainasua miguu yangu mtegoni.

16. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma,maana mimi ni mpweke na mnyonge.

17. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu;unitoe katika mashaka yangu.

18. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu;unisamehe dhambi zangu zote.

19. Angalia jinsi walivyo wengi maadui zangu;ona jinsi wanavyonichukia kwa ukatili.

20. Uyalinde maisha yangu, uniokoe;nakimbilia usalama kwako,usikubali niaibike.

21. Wema na uadilifu vinihifadhi,maana ninakutumainia wewe.

22. Ee Mungu, uwaokoe watu wako, Israeli;uwaokoe katika taabu zao zote.

Kusoma sura kamili Zaburi 25