14. Mwenyezi-Mungu ni rafiki ya wale wamchao;yeye huwajulisha hao agano lake.
15. Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima;yeye atainasua miguu yangu mtegoni.
16. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma,maana mimi ni mpweke na mnyonge.
17. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu;unitoe katika mashaka yangu.
18. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu;unisamehe dhambi zangu zote.
19. Angalia jinsi walivyo wengi maadui zangu;ona jinsi wanavyonichukia kwa ukatili.
20. Uyalinde maisha yangu, uniokoe;nakimbilia usalama kwako,usikubali niaibike.
21. Wema na uadilifu vinihifadhi,maana ninakutumainia wewe.
22. Ee Mungu, uwaokoe watu wako, Israeli;uwaokoe katika taabu zao zote.