Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 25:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, kwako naielekeza nafsi yangu!

2. Nakutumainia wewe, ee Mungu wangu,usiniache niaibike;adui zangu wasifurahie kushindwa kwangu.

3. Usimwache anayekutumainia apate aibu;lakini waaibike wote wanaokuasi kwa makusudi.

4. Unijulishe njia zako, ee Mwenyezi-Mungu;unifundishe nifuate unayotaka.

5. Uniongoze katika ukweli wako na kunifundisha,kwani wewe ni Mungu, mwokozi wangu;ninakutegemea wewe kila siku.

6. Uikumbuke huruma yako ee Mwenyezi-Mungu;uzikumbuke na fadhili zako kuu,ambazo zimekuwako tangu kale.

7. Usikumbuke dhambi na makosa ya ujana wangu;unikumbuke kadiri ya fadhili zako,kwa ajili ya wema wako, ee Mwenyezi-Mungu.

8. Mwenyezi-Mungu ni mwema na mnyofu,kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia.

9. Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu;naam, huwafundisha hao njia yake.

10. Mwenyezi-Mungu hutenda kwa fadhili na uaminifu,kwa wale wanaoshika agano lake na maamuzi yake.

11. Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu,unisamehe kosa langu kwani ni kubwa.

Kusoma sura kamili Zaburi 25