Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 24:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Dunia na vyote vilivyomo ni vyake Mwenyezi-Mungu;ulimwengu na wote waishio humo ni mali yake.

2. Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari;aliisimika imara juu ya mito ya maji.

3. Nani atakayepanda mlima wa Mwenyezi-Mungu?Nani atakayekaa katika hekalu lake takatifu?

4. Ni mtu wa matendo mema na moyo safi,asiyeuelekeza moyo wake katika upuuzi,wala kuapa kwa uongo.

5. Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu,na haki yake kwa Mungu mwokozi wake.

6. Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye;naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo.

7. Fungukeni enyi milango;fungukeni enyi milango ya kale,ili Mfalme mtukufu aingie.

8. Ni nani huyo Mfalme mtukufu?Ni Mwenyezi-Mungu, mwenye nguvu na uwezo;Mwenyezi-Mungu, mwenye uwezo vitani.

9. Fungukeni enyi malango,fungukeni enyi milango ya kale,ili Mfalme mtukufu aingie.

10. Ni nani huyo Mfalme mtukufu?Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi,yeye ndiye Mfalme mtukufu.

Kusoma sura kamili Zaburi 24