Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 22:7-19 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Wote wanionao hunidhihaki;hunifyonya na kutikisa vichwa vyao.

8. Husema: “Alimtegemea Mwenyezi-Mungu,basi, Mungu na amkomboe!Kama Mungu anapendezwa naye,basi, na amwokoe!”

9. Lakini ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,uliniweka salama kifuani pa mama yangu.

10. Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu.Tangu nilipozaliwa wewe umekuwa Mungu wangu.

11. Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia;wala hakuna wa kunisaidia.

12. Maadui wengi wanizunguka kama fahali;wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani!

13. Wanafunua vinywa vyao kama simba,tayari kushambulia na kurarua.

14. Nimekwisha kama maji yaliyomwagika;mifupa yangu yote imeteguka;moyo wangu ni kama nta,unayeyuka ndani mwangu.

15. Koo langu limekauka kama kigae;ulimi wangu wanata kinywani mwangu.Umeniacha kwenye mavumbi ya kifo.

16. Genge la waovu limenizunguka;wananizingira kama kundi la mbwa;wamenitoboa mikono na miguu.

17. Nimebaki mifupa mitupu;maadui zangu waniangalia na kunisimanga.

18. Wanagawana nguo zangu,na kulipigia kura vazi langu.

19. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami;ewe msaada wangu, uje haraka kunisaidia.

Kusoma sura kamili Zaburi 22