24. Maana yeye hapuuzi au kudharau unyonge wa mnyonge;wala hajifichi mbali naye,ila humsikia anapomwomba msaada.
25. Kwa sababu yako ninakusifukatika kusanyiko kubwa la watu;nitatimiza ahadi zangu mbele yao wakuchao.
26. Maskini watakula na kushiba;wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu watamsifu.Mungu awajalie kuishi milele!
27. Ulimwengu wote utakumbuka na kumrudia Mwenyezi-Mungu;jamaa zote za mataifa zitamwabudu.
28. Maana Mwenyezi-Mungu ni mfalme;yeye anayatawala mataifa.
29. Wenye kiburi wote duniani watasujudu mbele yake;wote ambao hufa watainama mbele yake,wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao.
30. Vizazi vijavyo vitamtumikia;watu watavisimulia habari za Mwenyezi-Mungu,
31. watatangaza matendo yake ya wokovu.Watu wasiozaliwa bado wataambiwa:“Mwenyezi-Mungu ndiye aliyefanya hayo!”