Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 22:10-29 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu.Tangu nilipozaliwa wewe umekuwa Mungu wangu.

11. Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia;wala hakuna wa kunisaidia.

12. Maadui wengi wanizunguka kama fahali;wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani!

13. Wanafunua vinywa vyao kama simba,tayari kushambulia na kurarua.

14. Nimekwisha kama maji yaliyomwagika;mifupa yangu yote imeteguka;moyo wangu ni kama nta,unayeyuka ndani mwangu.

15. Koo langu limekauka kama kigae;ulimi wangu wanata kinywani mwangu.Umeniacha kwenye mavumbi ya kifo.

16. Genge la waovu limenizunguka;wananizingira kama kundi la mbwa;wamenitoboa mikono na miguu.

17. Nimebaki mifupa mitupu;maadui zangu waniangalia na kunisimanga.

18. Wanagawana nguo zangu,na kulipigia kura vazi langu.

19. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami;ewe msaada wangu, uje haraka kunisaidia.

20. Iokoe nafsi yangu mbali na upanga,yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao!

21. Uniokoe kinywani mwa simba;iokoe nafsi yangu dhaifu toka pembe za nyati hao.

22. Nitawasimulia ndugu zangu matendo yako;nitakusifu kati ya kusanyiko lao:

23. Enyi mnaomcha Mwenyezi-Mungu, msifuni!Mtukuzeni enyi wazawa wote wa Yakobo!Mcheni Mungu enyi wazawa wote wa Israeli!

24. Maana yeye hapuuzi au kudharau unyonge wa mnyonge;wala hajifichi mbali naye,ila humsikia anapomwomba msaada.

25. Kwa sababu yako ninakusifukatika kusanyiko kubwa la watu;nitatimiza ahadi zangu mbele yao wakuchao.

26. Maskini watakula na kushiba;wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu watamsifu.Mungu awajalie kuishi milele!

27. Ulimwengu wote utakumbuka na kumrudia Mwenyezi-Mungu;jamaa zote za mataifa zitamwabudu.

28. Maana Mwenyezi-Mungu ni mfalme;yeye anayatawala mataifa.

29. Wenye kiburi wote duniani watasujudu mbele yake;wote ambao hufa watainama mbele yake,wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao.

Kusoma sura kamili Zaburi 22