Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 22:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Mbona uko mbali sana kunisaidia,mbali na maneno ya kilio changu?

2. Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu;napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati.

3. Hata hivyo, wewe ni mtakatifu;wewe watawala na kusifiwa na Waisraeli.

4. Wazee wetu walikutegemea;walikutegemea, nawe ukawaokoa.

5. Walikulilia wewe, wakaokolewa;walikutegemea, nao hawakuaibika.

6. Lakini mimi ni mdudu tu, wala si mtu;nimepuuzwa na kudharauliwa na watu.

7. Wote wanionao hunidhihaki;hunifyonya na kutikisa vichwa vyao.

8. Husema: “Alimtegemea Mwenyezi-Mungu,basi, Mungu na amkomboe!Kama Mungu anapendezwa naye,basi, na amwokoe!”

9. Lakini ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,uliniweka salama kifuani pa mama yangu.

10. Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu.Tangu nilipozaliwa wewe umekuwa Mungu wangu.

11. Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia;wala hakuna wa kunisaidia.

Kusoma sura kamili Zaburi 22