Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 2:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wanasema: “Tujiondoe katika utawala wao;tutupilie mbali minyororo yao!”

4. Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni,anawacheka na kuwadhihaki.

5. Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu,na kuwatisha kwa hasira, akisema:

6. “Nimemtawaza mfalme niliyemteua,anatawala Siyoni, mlima wangu mtakatifu!”

7. Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu.Mungu aliniambia:‘Wewe ni mwanangu,mimi leo nimekuwa baba yako.

8. Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako,na dunia nzima kuwa mali yako.

9. Utawaponda kwa fimbo ya chuma;utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’”

10. Sasa enyi wafalme, tumieni busara;sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia.

11. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji;

12. msujudieni na kutetemeka;asije akakasirika, mkaangamia ghafla;kwani hasira yake huwaka haraka.Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!

Kusoma sura kamili Zaburi 2